Jifunze Jinsi ya Kujenga Chanzo Kingine cha Kipato nje ya mshahara wako, Bila kuacha kazi unaoifanya kwa sasa.

Maisha ya kifedha hayategemei tu kiasi cha pesa unachopata, bali pia uwezo wako wa kujenga vyanzo vingine kwa ajili ya maisha yako ya baadaye.
 
Tanzania, watu wengi wanafanya kazi kwa bidii lakini bado wanakutana na changamoto ya kipato, maana kile wanachopata hakitosheleza mahitaji yao kwa asilimia 100%.
  • Mtumishi wa serikali anaweza kuwa na mshahara wa kila mwezi, lakini mahitaji ya familia yakaendelea kuongezeka.
  • Mfanyakazi wa private sector anaweza kufanya kazi kwa muda mrefu, lakini kipato chake kisitosheleze mipango yake.
  • Hata mfanyabiashara mdogo anaweza kufanya kazi kila siku lakini bado akashindwa kufikia kipato kinachotoshereza mahitaji yake.
  • Graduate anaweza kumaliza chuo na kutumia miaka kutafuta ajira bila kuingiza kipato chochote.
Hali hii inatufundisha jambo moja muhimu:
Kutegemea chanzo kimoja cha kipato kunatengeneza mipaka ya kufikia uhuru wa kifedha kwenye maisha.
 
Ndiyo maana watu wengi utafuta vyanzo vingine nya kipato, ujifunza biashara na ujuzi mbalimbali ili kujenga fursa mpya za kipato nje ya kazi zao wanazofanya.
 
Lakini swali ni hili
Je, ni lazima uwe na mtaji mkubwa, duka kubwa au uache kazi yako ili kuanza kujenga chanzo kingine cha kipato?
 
Siyo lazima kila mtu afanye hivyo.
Kuna aina mbalimbali za biashara ambazo mtu anaweza kujifunza na kuanza kufanya bila kulazimika kuacha kazi au ajila yake.
 
Mojawapo ni Network Marketing, aina ya biashara inayokupa nafasi ya kuunza bidhaa, kupitia njia ya mtandao wa watu na wewe unanufaika kwa mauzo unayofanya mwenyewe, pamoja na mauzo yanayofanywa na watu waliyo katika mtandao wako.
 
Lakini kabla hujafikiria kufanya hii biashara, kuna mambo muhimu unayopaswa kuyaelewa.
 
  • Network Marketing ni nini?
  • Ina tofauti gani na scam (Utapeli)?
  • Je, inaweza kufanya kazi Tanzania?
  • Je, unaweza kuijenga ukiwa bado una ajira au unatafuta ajira?
  • Na digital skills zinawezaje kukusaidia kuendesha biashara hii kwa urahisi zaidi?
Katika makala hii, nimekusudia uelewe kwanza Network marketing ni nini.
Kwa sababu uamuzi mzuri wa kuifanya biashara haupaswi kujengwa kwenye ahadi za mafanikio au utajiri wa haraka. Unapaswa kujengwa kwenye maarifa sahihi, uelewa wa kina

Tatizo la uhuru wa kifedha kwa watanzania wengi, halitokani na kutokufanya kazi kwa bidi.

Kufanya kazi kwa bidii ni muhimu, na waajiliwa wengi wanajitahidi sana kufanya kazi zao kwa bidi.
Lakini kuna tofauti kati ya kufanya kazi kwa bidii na kujenga kitu kinachoweza kukua kwa kadiri ya bidii unayowekeza.

 

Fikiria kila siku asubuhi
  • Mwalimu anaenda shule.
  • Nurse anaenda hospitalini.
  • Mtumishi wa serikali anaenda ofisini.
  • Mfanyakazi wa private sector anaendelea na kazi.
  • Mfanyabiashara anafungua biashara kila siku.
Wote wanafanya kazi kwa bidii.
Na mwisho wa mwezi wanapata mshahara
 
Lakini moja ya maajabu ya mshahara katika nchi zetu za Africa, uwa hauongezeki kuendana na kiwango cha juhudi unachowekeza hasa pale amabapo mtu ameajiliwa  serkalini au tasisi binafsi.
 
Lakini kila kukicha mahitaji yanaongezeka,
Mwanzoni ulikuwa unaishi peke yako
Lakini sasa umeoa una Watoto,
Hii inamaanisha mahitaji na majukumu yameongezeka lakini mshara uko pale pale au hata kama umeongezeka basi umeongezeka kwa kiwango kidogo sana.
Mahitaji yanakuwa kwa kasi kuliko kipato.
 
Ndiyo maana swali unalopaswa kujiuliza siyo tu “Nitawezaje kupata mshahara mkubwa?” unapaswa kujiuliza “Nitawezaje kujenga chanzo kingine cha kipato?”

Je, Unahitaji Kuacha Kazi Ili Uanze Biashara ?

Hapana.
Kama una ajira, usiache kazi yako kwa sababu tu umesoma makala hii.
 
Ajira inaweza kuwa sehemu muhimu ya maisha yako na inaweza kukupa msingi wa kujenga kitu kingine.
 
Unaweza kuanza kujifunza biashara baada ya kazi, mwisho wa wiki au kwa muda unaoweza kuutenga.
 
Lengo si kubadilisha maisha yako kwa siku moja.
Lengo ni kuanza kujenga kitu kingine hatua kwa hatua ambacho mwisho wa siku kitakupa uhuru wa kifedha.

Network Marketing Ni Nini?

Network Marketing
Ni biashara inayotumia bidhaa, wateja na mtandao wa watu kusambaza bidhaa au huduma.
 
Badala ya kampuni kutegemea maduka pekee, inaweza kutumia watu binafsi kusaidia kupeleka bidhaa kwa wateja.
 
Mtu anaweza kuwa mteja.
Katika mpango unaoruhusu, anaweza pia kuwa mshirika wa biashara, kuuza bidhaa na kujenga mtandao wa wasambazaji wengine.
Na malipo hutegemea mpango wa kampuni husika na mauzo yaliyofanywa na timu yako.
 
Lakini usiichukulie Network Marketing kama mashine ya kutengeneza pesa, kwa sababu tu umeona maisha ya kifahari ya watu wanaofanya biashara ya Network Marketing
 
Network Marketing ni biashara kama biashara zingine.
Na biashara inahitaji kujifunza upate ujuzi, kupata wateja, kujenga mahusiano, kufanya kazi na kuwa mvumilivu.

Je Network Marketing ni utapeli? Lakini Network Marketing ni ulaghai (Scam)?

Huenda hili ndilo swali lililopo kichwani mwako.
Ni swali zuri.
Siyo kila biashara inayotumia Network Marketing ni ulaghai (scam).
Na siyo kila fursa inayojiita Network Marketing ni halali.
 
Ndiyo maana unatakiwa kujifunza kutofautisha.
Usikubali kila kitu na usikatae kila kitu.
 
Chunguza kwanza.
Jinsi ya Kutambua Biashara Halali
Kabla hujatoa pesa yako, au kujiunga na timu yoyote ya Network Marketing jiulize:
  • Kuna bidhaa au huduma halisi katika kampuni?
  • Watu wananunua bidhaa kwa sababu wanazihitaji?
  • Kampuni iko wazi kuhusu gharama, bidhaa, masharti na malipo kwa wanachama wake?
  • Mapato yanategemea shughuli halisi za biashara na mauzo au yanategemea tu watu kujiunga na biashara?
  • Unaahidiwa utajiri wa haraka?
Ukiambiwa
“Jiunge leo, mwezi ujao utakuwa tajiri.”
Kuwa makini sana.
Biashara ya kweli inaweza kukua, lakini hakuna mtu anayepaswa kukuhakikishia utajiri wa haraka au ndani ya siku chache.
Usilipe kwa sababu umeshinikizwa presha.
Lipa kwa sababu umeelewa biashara.

Je, ninaweza kufanya Network Marketing nikiwa Tanzania?

Ili kuelewa hili, lazima tuangalie mazingira yetu.
Fikiria Mhitimu wa chuo.
Amemaliza chuo, uwezo anao na ana ndoto kubwa, lakini bado hajapata ajira.
 
Network Marketing haiwezi kuwa jibu la kila tatizo lake. Lakini inaweza kuwa moja ya fursa za kujifunza biashara na kujenga chanzo cha kipato, wakati akiendelea kutafuta ajira.
 
Fikiria Mwalimu, nurse, mfanyabiashara mdogo, mfanyakazi wa private sector ambaye mshahara wake hautoshelezi mahitaji yake.
Watu hawa wana kitu kimoja kinachofanana, hawana uhuru wa kifedha (Financial Freedom)
 
Wanahitaji kujifunza namna bora ya kutumia muda, ujuzi, mahusiano na teknolojia kunufaika na fursa ya Network Marketing na kujenga uhuru wa kiuchumi.
uwenda unajiuliza uhuru wa kifedha ni nini
 
Uhuru wa kifedha (Financial Freedom)
Ni kuwa na pesa za kutosha zinazokuwezesha kuishi maisha unayoyataka bila kulazimika kufanya kazi kila siku ili kulipa bili au kukidhi mahitaji ya msingi.
 
Lakini mafanikio katika network Marketing, hayaji kwa jina la biashara pekee.
Yanategemea bidhaa, soko, ujuzi, juhudi, muda na namna unavyoendesha biashara.

Network Marketing inafaa kwa mtu wa aina gani?

Network Marketing siyo biashara inayofanywa na  watu wasomi pekee.
  • Siyo lazima uwe umefika chuo kikuu.
  • Siyo lazima uwe mtaalamu wa biashara.
  • Siyo lazima ujue mambo yote ya teknolojia.
Kama unaweza kusoma na kuandika Kiswahili, kuelewa maelekezo na uko tayari kujifunza, unaweza kuanza kujifunza biashara hii.
  • Unaweza kuwa graduate.
  • Unaweza kuwa umeishia kidato cha nne au sita.
  • Unaweza kuwa na diploma.
  • Unaweza kuwa na degree.
  • Unaweza kuwa mwalimu, nurse, fundi, mfanyabiashara au mfanyakazi.
Elimu yako haipaswi kuwa sababu ya kuogopa kujifunza biashara.
Kinachokutofautisha ni utayari wa kujifunza na kutumia kile unachojifunza.

Digital Skills zinaweza kurahisisha Uendeshaji wa biashara ya Network Marketing?

Huenda ukasikia Digital Skills na ukafikiri:
“Mimi sijui computer. Hii biashara siwezi.”
  • Huhitaji kuwa programmer.
  • Huhitaji kujua coding.
  • Huhitaji kuwa mtaalamu wa teknolojia.
Unahitaji kuwa tayari kufundishwa & Kujifunza.
Unaweza kujifunza hatua kwa hatua:
  • Kutumia WhatsApp kuendesha biashara
  • Kutengeneza content au maudhui
  • Kutumia Facebook na Instagram kuendesha biashara
  • Kuwasiliana na wateja kwa namuna ambayo watavutiwa na kukusikiliza
  • Kutengeneza matangazo yenye uwezo wa kukuletea wateja kirahisi
  • Kutumia tuvuti (website), kukusanya taarifa za biashara yako sehemu moja.
  • Kutumia automation, kurahisisha shughuli mabalimbali za biashara
  • Kutumia tools za kidigitali kurahisisha kazi
Huhitaji kujua kila kitu leo.
Kile usichojua leo unaweza kujifunza na ukakijua.

Simu Yako Inaweza Kuwa nyenzo ya kuendesha Biashara.

Miaka iliyopita, mtu angeweza kutumia muda mwingi kutafuta wateja kwa kwenda nyumba kwa nyumba.
 
Lakini leo kuna  simu, WhatsApp, Facebook, Instagram kuna TikTok.
Unaweza kutengeneza video, kuandika maudhui, kufundisha na kujenga Hadhira yako (audience).
 
Hii imebadilisha sana namna ya kuendesha biashara katika karine hii ya mapinduzi ya tekinolojia ya mawasiliano.
 
Lakini kuwa na smartphone siyo sawa na kujua kuitumia kuendesha biashara.
Unahitaji ujuzi wa kuitumia, kuendesha biashara.

Digital Skills Zinakusaidiaje kuendesha biashara ya Network Marketing?

Network Marketing ya leo inaweza kufanywa kwa njia tofauti na zamani.
 
  • Badala ya kumtafuta kila mtu mmoja mmoja, unaweza kutengeneza maudhui (content) yanayowafikia watu wengi ndani ya muda mfupi.
  • Badala ya kueleza jambo lilelile kwa kila mtu, unaweza kutengeneza video, article au ebook ambayo mtu anaweza kujifunza wakati wowote.
  • Badala ya kutegemea marafiki wachache, unaweza kujenga Hadhira (audience) mpya kupitia internet au Mitandao ya kijamii.
Ndiyo maana ni muhimu kujifunza
  • Kutengeneza maudhui (Content)
  • Kutangaza biashara (Marketing)
  • Mitandao ya kijamii (social media)
  • Kupata wateja wanaoweza kununua (Lead Generation)
  • Kuuza bidhaa au huduma (Sales)
  • Kuwafuatilia wateja (Follow-up)
  • Kufanya kazi kiotomatiki (Automation)
Si kwa sababu teknolojia itafanya biashara yote kwa niaba yako, bali kwa sababu inaweza kukusaidia kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Fikiria Miaka Miwili Kutoka Leo (siku amabayo umesoma Makala hii)

Usifikirie tu mwisho wa mwezi huu nitakuwa nimefanikiwa kwa kiasi gani.
 
Jiulize
“Nikianza kujifunza leo na kuendelea kujenga kwa miaka 1, 2 au 5, nitakuwa nimejenga biashara kwa ukubwa kiasi gani?”
  • Unaweza kujenga ujuzi.
  • Unaweza kujenga wateja.
  • Unaweza kujenga hadhira (audience).
  • Unaweza kujenga brand.
  • Unaweza kujenga community.
  • Unaweza kujenga timu imara.
  • Unaweza kujenga uzoefu wa biashara.
Hivi ni vitu ambavyo vinaweza kuwa na thamani kwa muda mrefu.
Ndiyo maana usiangalie Network Marketing kwa swali la “Nitapata nini wiki hii?”
Jiulize “Ninaweza kujenga nini kwa muda mrefu?”

Usijiunge Kwa Sababu Tu Nimekuambia

Mimi, Joctan Motoka, nataka ujifunze Network Marketing.
 
Lakini sitaki ujiunge kwa sababu tu nimekuambia “Utapata pesa nyingi.”
 
  • Sitaki kukushawishi kwa picha za magari ya kifahari.
  • Sitaki kukuahidi kwamba ndani ya siku 30 maisha yako yatabadilika.
Nataka ufanye kitu tofauti kabisa
Ujifunze kwanza.
  • Elewa biashara kwa undani.
  • Elewa bidhaa utakazouza.
  • Elewa wateja wako watakuwa wa aina gani, wanatabia gani, wanaamini nini. Maana ukimuelewa mteja wako inaukuwa rahisi sana kumuuzia.
  • Elewa gharama ya bidhaa na kiwango cha faida utakachokipata kutoka katika hiyo bidhaa.
  • Elewa namna malipo yanavyofanyika baada ya kazi.
  • Elewa kazi inayotakiwa kufanywa.
Kisha fanya uamuzi.
Huu ndiyo unapaswa kuwa mtazamo wa mtu anayefikiria kujenga biashara ya Network Marketing yenye mafanikio makubwa.

Anza Kujifunza biashara na kuelewa biashara.

Huenda bado hujui kama Network Marketing ni kwa ajili yako.
Hakuna tatizo.
Usianze kwa kutoa pesa. Anza kwa kujifunza.
  • Jifunze Network Marketing.
  • Jifunze tofauti kati ya biashara halali na scam.
  • Jifunze namna ya kupata wateja.
  • Jifunze namna ya kujenga team.
  • Jifunze digital marketing.
  • Jifunze social media.
  • Jifunze automation.
Kisha fanya uamuzi wako.
Nimeweka mafunzo ya bure kwenye:
www.joctanmotoka.com

Anza Na Hatua Hizi 5

01. Jiunge na Kozi Bure

Anza kujifunza Network Marketing hatua kwa hatua, chini ya usimamizi wa walimu wabobezi na wenye uzoefu klatika biashara ya Network Marketing

02. Download eBooks Zetu Bure

Jifunze zaidi kuhusu biashara, mauzo, marketing, Network Marketing na digital skills.
Maneno yanaweza kukuza biashara yako au kuua bishara yako,
Jifunze mbinu za kuandika Ujumbe Unaovutia Umakini, unaojenga Uamininifu na Kuwageuza Wasomaji kuwa wateja

03. Jifunze Digital Skills

Jifunze kutumia teknolojia kurahisisha namna unavyotafuta wateja na kuendesha biashara.

04. Jiunge na Timu Yetu

Baada ya kujifunza na kuona kwamba Network Marketing ni njia inayokufaa, unaweza kujiunga na timu yetu na kuanza kujenga pamoja nasi.

05. Jiunge na Community Yetu

Usijifunze peke yako. Kuwa sehemu ya watu wanaojifunza, wanaoshirikiana na wanaojenga biashara.

Neno langu kwako

  1. Kama wewe ni graduate ambaye bado unasubiri ajira…
  2. Kama wewe ni mwalimu anayehisi mshahara hautoshi…
  3. Kama wewe ni nurse anayefanya kazi kwa bidii lakini bado ana mahitaji mengi…
  4. Kama wewe ni mtumishi wa serikali…
  5. Kama wewe ni mfanyakazi wa private sector…
  6. Au kama wewe ni mfanyabiashara mdogo unayetafuta namna ya kukua…
Makala hii nimeiandika kwa ajili yako.
Sikwambii kwamba Network Marketing ni biashara ya miujiza kwamba utafanikiwa ndani ya wiki moja.
Wala sikwamba uache kazi yako.
Ninachokwambia ni hiki:
Anza kujifunza njia mpya ya kujenga kipato.
 
Usikatae kabla hujaelewa na.
Usikubali kabla hujachunguza kwa undani.

Jifunze kwanza, Kisha amua.

Kwa sababu huwezi kujenga maisha tofauti kwa kutumia maarifa yale yale yaliyo kufanya kuwa na maisha uliyo nayo sasa.
 
Unahitaji kujifunza ujuzi utakao kusaidia kuendesha biashara ya Network Marketing kwa njia rahisia na namuna bora zaidi itakayo kupa matokeo (Hustle smarter)
 
Hatua yako inayofuata siyo kutafuta mshahara mwingine.
Ni  kujifunza jinsi ya kujenga biashara yako mwenyewe.
 
Mimi ni Joctan Motoka, na kama uko tayari kuanza kujifunza, ninakukaribisha nimekuandalia free course  utakayojifunza katika tuvuti hii.
Na baada ya kuelewa Network Marketing vizuri, kama utaona ni safari inayokufaa:
Jiunge na timu yetu, tujenge pamoja.
Anza kujifunza ujuzi utakao kusaidia kuendesha biashara kirahisi na kwa mafanikio makubwa (Hustle Smarter with Joctan Motoka).
Picture of Joctan Motoka

Joctan Motoka

Digital Marketing Expert I Creative Graphics Designer
Author I Trainer I Network Marketer
Online Entrepreneur

Ninasaidia watu na biashara kutumia ujuzi na teknolojia kufikia wateja wengi zaidi, kuongeza mauzo na kuendesha biashara kwa mfumo bora zaidi.

Bofya Butoni hapo chini kuwasiliana Nasi

Zaidi ya mshahara

Kitabu hiki kinajibu maswali matatu ambayo uwenda na wewe umekuwa ukijiuliza kwa muda mrefu bila kupata majibu, na kutoa mwongozo wa hatua za kuchukua kujenga kipato kingine nje ya mshahara wako.
  1. Kwa nini chanzo kimoja cha kipato huwa hakitoshi?
  2. Je, kweli inawezekana kujenga kipato cha ziada bila
    kuacha kazi yako?
  3. Kwa nini watu wengine ufanikiwa kwenye network
    marketing na wengine ukata tamaa, kabla ya
    kufanikiwa?

Jifunze jinsi ya kutumia ujuzi wa kidigitali kurahisisha Biashara yako ya Network Marketing

Siyo kwamba Biashara ya Network Marketing haifanyi kazi au ni Ngumu.
Bali ni mfumo au njia unazotumia kuendesha Biashara, ndizo hazikupi matokeao.
Maana zimepitwa na wakati/ hazifanyi kazi kwa sasa.

Karibu Tuzungumze Kuhusu, Biashara ya Network Marketing

Pata vitabu na Miongozo mbalimbali itakayo kusaidia, kubadilisha Biashara yako Mtandaoni

Subscribe uzidi kupata Taarifa zetu zaidi kwa kujaza fomu hapa chini

    Scroll to Top