About Me

Ninasaidia biashara kutumia teknolojia, Masoko ya Kidigitali (Digital Marketing) na mifumo bora kuwafikia wateja wengi zaidi, kuongeza mauzo na kufanya kazi kwa ufanisi.

Karibu kwenye tovuti ya Joctan Motoka.

Mimi ni Joctan Motoka,
      • Mtaalamu wa Masoko ya Kidigitali (Digital Marketing),
      • Mwandishi wa vitabu,
      • Mkufunzi wa maswala ya biashara mtandaoni,
      • Mjasiriamali wa mtandaoni,
      • Network Marketer na
      • Creative Graphics Designer.
Nimejikita katika kusaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati, wajasiriamali, Network Marketers na kampuni kutumia ujuzi, teknolojia na mifumo ya kisasa kuboresha namna wanavyo wafikia wateja, kufanya mauzo na kuendesha biashara zao.
Kwa sababu leo, kuwa na bidhaa au huduma nzuri pekee haitoshi.
Unahitaji pia kujua jinsi ya kuwafikia watu sahihi, kuwafanya waielewe biashara yako, kujenga uaminifu, kufuatilia wanaovutiwa na kuwageuza fursa kuwa mauzo.
Hapo ndipo ninapolenga kusaidia.

Maono Yetu (Our Vision)

Kuwawezesha vijana wa Tanzania kujenga maisha bora kupitia ujuzi wa kidigitali na biashara za kisasa.
Tunaamini teknolojia imefungua fursa mpya za kujifunza, kufanya kazi, kujiajiri na kujenga biashara.
Maono yetu ni kuona vijana wengi zaidi wakiwa na
  1. Ujuzi,
  2. Maarifa na
  3. Uwezo wa kutumia teknolojia
Kujipatia kipato na kuendesha biashara zao kwa njia ya kitaalamu, yenye ufanisi na inayoendana na mahitaji ya biashara za kidigitali za karne ya 21.

Dhamira Yetu (Our Mission)

Kuwajengea vijana uwezo wa kutumia ujuzi wa kidigitali kujipatia kipato, kujenga biashara na kukuza biashara zao kwa mfumo unaoendana na dunia ya teknolojia.
Tunafanikisha dhamira hii kupitia
      1. Mafunzo,
      2. Vitabu
      3. Miongozo
      4. Kozi za Mtandaoni
      5. Maudhui ya Kielimu
      6. Mentorship
Tunaweka mkazo kwenye ujuzi kama:
      • Digital Marketing
      • Copywriting
      • Mauzo (Sales)
      • Follow-Up
      • Social Media
      • Automation
      • Website
      • Personal Branding
      • Online Business
Lengo si kuwafanya vijana wajue teknolojia pekee.
Lengo ni kuwasaidia kutumia ujuzi huo katika kutengeneza fursa za kipato, kupata wateja, kuongeza mauzo na kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi.

Lengo Letu Hadi 2030

Kufikia mwaka 2030, tuna lengo la kuwafikia na kuwawezesha angalau vijana 4,000 nchini Tanzania kupata ujuzi wa kidigitali unaoweza kuwasaidia
      • Kujenga vyanzo vya kipato
      • Kuanzisha au kukuza biashara
      • Kuwafikia wateja kupitia njia za kidigitali
      • Kuongeza fursa za mauzo
      • Kutumia teknolojia kupunguza kazi zinazojirudia
      • Kuendesha biashara kwa mfumo na ufanisi
      • Kujenga biashara zinazoendana na mahitaji ya karne ya 21
Kwa kifupi, tunataka kusaidia vijana wasiwe watumiaji wa teknolojia pekee, bali waweze kuitumia teknolojia kujenga fursa, kipato na biashara zao.
 

Tunachoamini

  • Ujuzi unaweza kufungua fursa.
  • Teknolojia inaweza kuongeza uwezo.
  • Mfumo unaweza kuongeza ufanisi.
  • Na utekelezaji unaweza kuleta matokeo.
Ndiyo maana tunahamasisha vijana
Kujifunza, kutekeleza, Kuboresha, na kukuza biashara zao kwa kutumia ujuzi wa kidigital.
Kwa sababu tunataka kuona kizazi cha vijana kinachoweza kujiajiri, kujipatia kipato na kujenga biashara zinazoweza kushindana katika dunia ya kidigitali ya karne ya 21.

Biashara yako inahitaji nini ili ikue?

Kila mfanyabiashara anataka kuona biashara yake ikikua.
Anataka kuona
      • Wateja wengi zaidi.
      • Mauzo mengi zaidi.
      • Faida nzuri zaidi.
      • Na biashara inayoweza kuendeshwa kwa ufanisi zaidi.
Lakini kufikia hapo kunahitaji zaidi ya kufanya kazi kwa bidii kila siku.
Unahitaji mfumo unaokusaidia kujua
      • Utawafikiaje wateja?
      • Utawafikia wapi?
      • Utawaambia nini?
      • Utawajengeaje uaminifu?
      • Utawafuatiliaje?
      • Utawasaidiaje kufanya uamuzi wa kununua?
      • Na ni kazi zipi zinaweza kufanywa na teknolojia kwenye biashara yako?
Ndiyo maana kazi yangu inalenga kuunganisha ujuzi wa biashara, masoko, mauzo na teknolojia katika mfumo unaoweza kutumika kuendesha Biashara.

Sio kufanya kazi zaidi. Ni kufanya kazi kwa mfumo bora.

Ninaamini kufanya kazi kwa bidii ni muhimu.
Lakini biashara inapokua, huwezi kuendelea kuongeza mzigo wa kazi kila siku bila kuboresha namna unavyofanya kazi.
      • Kuna kazi zinazojirudia.
      • Kuna mawasiliano yanayorudiwa.
      • Kuna ufuatiliaji wa wateja (Follow-Up).
      • Kuna taarifa zinazohitaji kupangwa.
      • Kuna maudhui yanayohitaji kutengenezwa.
Baadhi ya kazi hizi zinaweza kusaidiwa na teknolojia na Automation.
Lengo ni kukusaidia kutumia teknolojia pale inapoweza
      1. Kuokoa muda.
      2. Kupunguza kazi zinazojirudia.
      3. Kuboresha mpangilio wa kazi.
      4. Kusaidia ufuatiliaji wa wateja.
      5. Kurahisisha mchakato wa mauzo.
      6. Na kukupa nafasi ya kuzingatia mambo muhimu zaidi ya biashara.
Teknolojia isiwe mzigo mwingine. Itumike kuwa sehemu ya mfumo wa biashara yako.

Ninawasaidia kina nani?

Wafanyabiashara wadogo, wa kati na makampuni
Ikiwa una biashara na unataka kupata wateja wengi zaidi, kuongeza mauzo na kutumia teknolojia vizuri, tunalenga kukusaidia kujenga msingi bora wa biashara ya kidigitali.
WAJASIRIAMALI
Ikiwa una bidhaa, huduma au biashara unayojenga, tunakusaidia kuelewa namna ya kutumia maarifa ya masoko, mauzo na teknolojia kufikia watu wengi zaidi.
NETWORK MARKETERS
Ikiwa unafanya Network Marketing na unataka kuacha kutegemea kusumbua watu bila mpangilio, tunakufundisha namna ya kutumia ujuzi wa kidigitali kujenga biashara yako kwa njia ya kisasa.
KAMPUNI
Ikiwa kampuni yako inahitaji kufikia watu wengi zaidi, kujenga uwepo mzuri mtandaoni, kuboresha mawasiliano na wateja au kuimarisha mfumo wa masoko na mauzo, tunaweza kufanya kazi pamoja.

Huduma na ujuzi tunaotoa

Tunasaidia biashara kuelewa na kutumia njia mbalimbali za kidigitali kuwafikia wateja.
Tunazingatia mambo kama:
  • Mitandao ya kijamii
  • Maudhui (Content)
  • Matangazo ya mtandaoni
  • Ujenzi wa chapa (Branding)
  • Utafutaji wa wateja (Follow- Up)
  • Mikakati ya mauzo (Sales Strategies)
Lengo ni kusaidia biashara yako kufika mbele ya watu sahihi na kuongeza fursa za kupata wateja.
Mteja hawezi kununua kile asichokielewa.
Ndiyo maana namna unavyoandika na kuwasilisha ujumbe wa biashara yako ni muhimu.
Tunasaidia katika kuandaa:
  • Matangazo
  • Machapisho ya mitandao ya kijamii
  • Ujumbe wa WhatsApp
  • Kurasa za mauzo
  • Maelezo ya bidhaa
  • Maelezo ya huduma
  • Barua pepe
  • Maudhui ya tovuti
Lengo ni kufanya biashara yako ieleweke, ionekane kuwa na thamani na kumsaidia mteja kuchukua hatua.
Sio kila mtu atanunua mara ya kwanza.
  • Mtu anaweza kuuliza bei.
  • Akaomba taarifa.
  • Akaonyesha kuvutiwa.
  • Halafu akaondoka bila kununua.
Hapo ndipo ufuatiliaji unapokuwa muhimu.
Tunafundisha namna ya
  • Kuwasiliana na mteja kwa wakati
  • Kumkumbusha bila kumsumbua
  • Kutoa taarifa yenye thamani
  • Kuendelea kujenga uaminifu
  • Kufuatilia fursa za mauzo
  • Kuwa na mpangilio wa mawasiliano
Badala ya kupoteza watu wanaovutiwa, jenga mfumo wa kuendelea kuwasiliana nao kwa njia sahihi.
Biashara nyingi hupoteza muda kwenye kazi zinazojirudia.
Automation inaweza kusaidia baadhi ya kazi hizo kufanyika kwa mfumo.
Tunashirikisha maarifa kuhusu namna teknolojia inaweza kusaidia katika:
  • Mawasiliano
  • Ufuatiliaji wa wateja
  • Kukusanya taarifa
  • Kuhifadhi taarifa
  • Kutuma taarifa
  • Kupanga kazi
  • Kusimamia mchakato wa mauzo
Lengo ni kufanya biashara yako ifanye kazi kwa mpangilio zaidi na kupunguza mzigo wa kazi zisizo za lazima.
Tovuti ni sehemu muhimu ya uwepo wa biashara mtandaoni.
Tunasaidia kujenga tovuti zinazomsaidia mgeni:
  • Kuelewa biashara yako.
  • Kujua bidhaa au huduma zako.
  • Kujenga uaminifu.
  • Na kuchukua hatua.
Tovuti inaweza kusaidia biashara:
  • Kuonyesha bidhaa
  • Kuonyesha huduma
  • Kupokea mawasiliano
  • Kushiriki maudhui
  • Kupokea maombi
  • Kuuza mtandaoni
  • Kujenga uwepo wa kitaalamu
Tovuti nzuri siyo mapambo tu. Inapaswa kusaidia biashara kufanya kazi.
Kuwa na ukurasa wa biashara pekee haitoshi.
Unahitaji kujua utachapisha nini, kwa nani, kwa sababu gani na unataka mtu afanye nini baada ya kuona maudhui yako.
Tunasaidia katika.
  • Kupanga maudhui (Content planning)
  • Kuandika machapisho (Social media posts)
  • Kusimamia kurasa (Social Media Management)
  • Kujenga mahusiano na watazamaji
  • Kuandaa maudhui yenye lengo la biashara
Lengo si kuchapisha tu. Lengo ni kutumia mitandao ya kijamii kusaidia biashara yako kukua.
Muonekano wa biashara yako una nafasi katika namna watu wanavyoiona.
Tunatoa huduma zinazohusiana na:
  • Graphics Design
  • Branding
  • Printing ya (Mabango, Brochures, Flyers, Posters, Banners, Product catalogues, company profiles, branded notebooks, stickers, labels, and other promotional materials).
Tunasaidia biashara kuwasilisha ujumbe wake kwa muonekano unaoendana na biashara yake.
Maarifa yana thamani zaidi unapoweza kuyatumia.
Ndiyo maana ninaandaa mafunzo yanayolenga kukusaidia kuelewa na kutumia ujuzi wa biashara ya kisasa.
Mafunzo yanahusisha:
  1. Digital Marketing
  2. Copywriting
  3. Sales
  4. Follow-Up
  5. Social Media
  6. Automation
  7. Network Marketing
  8. Online Business
  9. Personal Branding
Na teknolojia nyingine za biashara.
Baadhi ya mafunzo yanapatikana bure, na mengine ni mafunzo ya kina yanayolipiwa.
Jifunze kile unachohitaji. Kisha kiweke kwenye vitendo.

Jifunze bure kupitia maudhui yetu

Ninaendelea kushiriki maarifa kupitia tovuti yangu:
www.joctanmotoka.com
Hapa utapata makala, mawazo, miongozo na maudhui kuhusu:
      • Biashara
      • Digital Marketing
      • Mauzo
      • Copywriting
      • Social Media
      • Automation
      • Network Marketing
      • Teknolojia
      • Online Business
Anza na maudhui ya bure na ujifunze hatua kwa hatua.

Subscribe youtube channel yetu

Tunatumia YouTube kushiriki mafunzo na maarifa ambayo yanaweza kukusaidia kuelewa biashara na teknolojia kwa njia rahisi.
Kama unapenda kujifunza kupitia video:
Subscribe channel yetu ya YouTube na endelea kujifunza nasi.

Tufollow kwenye mitandao yetu ya kijamii

Tunashiriki maudhui kuhusu biashara, masoko, mauzo, teknolojia na ujuzi mwingine wa kidigitali.
Tufuate ili usikose:
      1. Mafunzo mapya.
      2. Makala
      3. Video
Na maarifa ya kukusaidia kuboresha biashara yako.

Unataka kuanza wapi?

Hatua yako inayofuata ni rahisi

Huhitaji kuanza kila kitu kwa wakati mmoja.
Chagua kile unachohitaji sasa.
Jifunze, Tekeleza, Pima, Boresha na Endelea kukua.
Kwa sababu biashara bora haijengwi kwa kufanya kila kitu kwa wakati mmoja. Inajengwa kwa kufanya jambo sahihi, kwa mfumo sahihi, na kuliboresha kila siku.

Tupo tayari kuongea kuhusu biashara yako?

Ikiwa una biashara, kampuni, unafanya Network Marketing, unataka kujifunza au unahitaji huduma ya kidigitali, tungependa kusikia kutoka kwako.
Tuambie
      • Unachofanya
      • Changamoto uliyonayo.
      • Unachotaka kufikia.
Na tunaweza kuangalia namna ya kufanya kazi pamoja.
Wateja zaidi, Mauzo zaidi, Mfumo bora wa biashara.
Picture of Joctan Motoka

Joctan Motoka

Digital Marketing Expert I Creative Graphics Designer
Author I Trainer I Network Marketer
Online Entrepreneur

Ninasaidia watu na biashara kutumia ujuzi na teknolojia kufikia wateja wengi zaidi, kuongeza mauzo na kuendesha biashara kwa mfumo bora zaidi.

Bofya hapa Kunipigie

Karibu Tuzungumze Kuhusu, Biashara

Jifunze jinsi ya kutumia ujuzi wa kidigitali kuendesha Biashara yako ya Network Marketing Bure

Si kwamba Biashara ya Network Marketing haifanyi kazi au ni Ngumu.
Bali ni mfumo au njia unazotumia kuendesha Biashara, ndizo hazikupi matokeao.
Maana zimepitwa na wakati/ hazifanyi kazi.

Some of My Story

Subscribe uzidi kupata Taarifa zetu zaidi kwa kujaza fomu hapa chini

    Scroll to Top