Huenda una bidhaa nzuri.
Unaweza kutengeneza video nzuri.
Unaweza kupiga picha nzuri.
Unaweza kuwa na ukurasa mzuri wa Facebook au Instagram.
Lakini bado…
Unapost mara kwa mara lakini watu wachache wanaona.
Unaweka pesa kwenye matangazo lakini hujui kama zinakuletea faida.
Unapata views na likes, lakini si wateja.
Unaongeza budget lakini mauzo hayaongezeki.
Unabadilisha picha, video na maandishi bila kujua ni kitu gani hasa kinachofanya tangazo lifanye kazi.
Hujui ni wateja gani unaowalenga na kwa nini.
Unasikia kuhusu Pixel, Retargeting, Testing, Metrics, Scaling lakini hujui vinafanya kazi vipi.
Wakati mwingine unapata mteja mmoja, wakati mwingine hakuna kabisa.
Unahisi biashara yako inahitaji “bahati” ili tangazo lipate wateja.
Lakini je, kweli tatizo ni biashara yako?
Huenda si bidhaa yako.
Huenda ni namna unavyotumia matangazo yako.
Na hapo ndipo kila kitu kinaanza kubadilika…
Watu wengi wanaweza kuwekaza pesa kwenye Facebook au Instagram.
Lakini wachache wanajua:
Wanamlenga nani.
Wanapaswa kusema nini.
Ni video au picha gani itumike.
Waweke pesa kiasi gani.
Wapime nini.
Wajueje kama tangazo linafanya kazi.
Wabadilishe nini pale matokeo yanapokuwa mabaya.
Na waongezeje bajeti pale tangazo linapoanza kufanya vizuri.
Kwa sababu hiyo…
Meta Ads si kubofya tu kitufe cha “Boost Post”.
Ni kujua unachofanya na kwa nini unakifanya.
NGOME YA BIASHARA ZA KIDIGITALI ni mwongozo wa kukusaidia kuelewa kwa kina misingi muhimu ya kutumia matangazo ya kulipia mtandaoni kupitia Meta Ads.
Kitabu hiki hakilengi kukufundisha kuweka tangazo tu.
Kinalenga kukusaidia kuelewa mfumo mzima.
Kwa nini tangazo linafanya kazi?
Kwa nini halifanyi kazi?
Ni watu gani wanapaswa kuliona?
Ni taarifa gani zinapaswa kuangaliwa?
Na ni hatua gani unapaswa kuchukua baada ya kuona matokeo?
Ndani ya kitabu hiki utajifunza mambo muhimu kama:
Jinsi ya kumfikia mteja sahihi
Badala ya kutangaza kwa kila mtu, utajifunza umuhimu wa kumwelewa mtu unayetaka kumfikia na namna ya kutumia walengwa sahihi.
Jinsi ya kuelewa kinachomfanya mteja achukue hatua
Mteja haangalii tu bidhaa.
Anaangalia kama ujumbe wako unamhusu, kama anaweza kukuamini na kama anapata sababu ya kuchukua hatua.
Utajifunza misingi ya saikolojia ya mteja na namna inavyohusiana na matangazo.
Video nzuri peke yake haitoshi
Unaweza kutengeneza video nzuri sana.
Lakini kama haimfikii mtu sahihi au ujumbe wake haumvutii, inaweza kupita bila kuleta mauzo.
Utajifunza jinsi ya kuunganisha video, picha na ujumbe na mfumo wa matangazo.
Jinsi ya kutumia pesa za matangazo kwa ufahamu
Usiweke pesa kwa sababu tu watu wengine wanaweka.
Elewa bajeti, matumizi na namna ya kufanya maamuzi kutokana na matokeo unayoyaona.
Jinsi ya kusoma namba za tangazo
Likes na views pekee hazitoshi.
Utajifunza kuelewa vipimo vya matangazo (Metrics) vinavyokusaidia kuona kinachoendelea na kutambua sehemu ya tangazo lako inayohitaji kuboreshwa.
Jinsi ya kugundua tangazo linalofanya kazi na lisilo fanya kazi
Usibashiri.
Jifunze kujaribu matoleo tofauti ya matangazo (Testing) ili kugundua ujumbe, picha, video au walengwa wanaofanya vizuri zaidi.
Jinsi ya kufuatilia watu walivutiwa na biashara yako
Utaelewa Meta Pixel, kwa nini ni muhimu na jinsi inavyokusaidia kufuatilia vitendo vya watu kwenye tovuti yako.
Usiwaache watu waliokwishakuona
Mtu anaweza kuona tangazo lako leo na asinunue.
Haimaanishi kwamba hana interest.
Utajifunza dhana ya kuwafikia tena watu (Retargeting) ambao tayari waliwahi kuonyesha nia kwenye biashara yako.
Ukipata kinachofanya kazi, jifunze jinsi ya kukikuza
Tangazo likianza kufanya vizuri, hatua inayofuata si kuongeza pesa bila mpango.
Utajifunza misingi ya kukuza kampeni (Scaling) kwa kutumia taarifa na matokeo.
Huenda umeandaa video nzuri.
Umeandika ujumbe mzuri.
Umeweka pesa.
Lakini bado hakuna mauzo.
Kwa nini?
Kwa sababu tangazo ni sehemu moja tu ya safari ya mteja.
Mtu anaweza:
Kuona tangazo lako.
Kusoma ujumbe wako.
Kuangalia video.
Kubofya.
Kufika kwenye ukurasa wako.
Kukutumia ujumbe.
Kuuliza bei.
Kufikiria.
Na hatimaye kuamua kununua au kuondoka.
Kila hatua inaweza kuongeza au kupunguza nafasi ya kupata mteja.
Ndiyo maana unahitaji kuelewa mfumo mzima, si tangazo pekee.
Mteja wa leo
Anaona biashara nyingi.
Anaona video nyingi.
Anaona ofa nyingi.
Anaona matangazo kila anapofungua simu yake.
Na ndani ya sekunde chache anaweza kuamua “Nisome.” au “Nisogeze.”
Kwa hiyo, kama mfanyabiashara wa mtandaoni, unahitaji kuelewa
Nini kinamvuta?
Nini kinamfanya asikilize?
Nini kinamfanya akuamini?
Na nini kinamfanya achukue hatua?
Hapo ndipo maarifa ya Meta Ads, uandishi wa mauzo na saikolojia ya mteja yanapoungana.
Badala ya kuangalia tu kama watu wamependa tangazo…
Unaanza kujiuliza
Ni watu gani wamefikiwa?
Wamefanya nini?
Nimepata matokeo gani?
Nitumie bajeti gani?
Nibadilishe nini?
Niendelee au nisitishe?
Ninawezaje kuboresha?
Hapo ndipo unapoanza kuondoka kwenye kubahatisha na kuanza kufanya maamuzi kwa kutumia taarifa.
Ndani ya NGOME YA BIASHARA ZA KIDIGITALI unapata mwongozo utakaokusaidia kuelewa na kutumia matangazo ya kulipia kwa njia inayoweza kukusaidia
Kupata wateja zaidi,
Kupunguza matumizi yasiyo na mpango na
Kukuza biashara yako.
Kitabu hiki kinakufundisha mambo muhimu 11 ambayo yanaweza kubadilisha namna unavyotangaza biashara yako tandaoni
Walengwa (Audience)
Utajua jinsi ya kumfikia mtu sahihi, badala ya kuonyesha tangazo lako kwa kila mtu.
Hii inakusaidia kutumia pesa zako kufikia watu ambao wana uwezekano mkubwa wa kuhitaji bidhaa au huduma yako.
Ujumbe wa Tangazo
Utajua jinsi ya kuandaa ujumbe ambao mteja anaweza kuuelewa haraka na kuona sababu ya kuchukua hatua.
Hii inakusaidia kufanya tangazo lako lisomeke kwa urahisi na kumfanya mteja awe na hamu ya kujua zaidi kuhusu kile unachouza.
Video na Picha
Utajua jinsi ya kutumia picha na video zinazovuta umakini na kueleza bidhaa au huduma yako kwa njia rahisi.
Badala ya tangazo lako kupita tu mbele ya macho ya watu, utajifunza jinsi ya kulifanya lisimamishe macho na umakini wa mteja.
Bajeti
Utajua jinsi ya kupanga pesa zako za matangazo kwa uangalifu.
Hii inakusaidia kuepuka kutumia pesa bila kujua zinakuletea nini na kukupa uwezo wa kuendesha matangazo kulingana na uwezo wa biashara yako.
Vipimo vya Matangazo (Metrics)
Utajua ni namba zipi muhimu za kuangalia ili kuelewa kama tangazo lako linafanya kazi au linapoteza pesa.
Hivyo, utaweza kuona kinachoendelea na kufanya maamuzi kwa kutumia matokeo badala ya kubahatisha.
Kujaribu Matangazo (Testing)
Utajifunza jinsi ya kujaribu mawazo tofauti kwenye matangazo yako na kuona lipi linafanya vizuri zaidi.
Hii inakusaidia kuacha kutegemea tangazo moja tu na badala yake kugundua njia zinazoweza kukuletea matokeo bora.
Meta Pixel
Utajifunza jinsi ya kutumia Meta Pixel kupata taarifa kuhusu watu wanaofanya vitendo kwenye tovuti yako baada ya kuona matangazo.
Taarifa hizi zinaweza kukusaidia kuelewa zaidi tabia za watu wanaovutiwa na biashara yako na kufanya matangazo yako kwa uelewa zaidi.
Kuwafikia Tena Wateja (Retargeting)
Utajifunza jinsi ya kuwafikia tena watu ambao
Tayari waliona tangazo lako,
Walitembelea tovuti yako au
Walionyesha interest kwenye biashara yako.
Kwa sababu si kila mtu hununua mara ya kwanza, hii inakupa nafasi nyingine ya kumkumbusha mteja na kumrudisha kwenye biashara yako.
Kukuza Kampeni (Scaling)
Unapogundua tangazo linalofanya vizuri, utajifunza jinsi ya kulikuza kwa mpango.
Hii inakusaidia kuongeza juhudi kwenye kile kinachofanya kazi badala ya kuongeza pesa kwa kubahatisha na kupoteza pesa zako kwa kitu kisicho na matokeo.
Uchambuzi wa Matokeo
Utajifunza jinsi ya kusoma matokeo ya matangazo yako na kujua
Kilichofanya kazi,
Kisichofanya kazi na
Kile kinachohitaji kubadilishwa.
Kwa kufanya hivyo, kila kampeni inaweza kukupa somo la kukusaidia kufanya kampeni inayofuata vizuri zaidi.
Mfumo wa Kuboresha Matangazo
Utajenga mfumo wa kuangalia matangazo yako, kuona kinachohitaji kubadilishwa na kuendelea kuyaboresha hatua kwa hatua.
Hii inakusaidia kuacha kutangaza kwa kubahatisha na kuanza kuwa na njia ya kufanya matangazo yako yawe bora kadiri unavyopata matokeo mapya.
Utakuwa umeelewa jinsi ya kumfikia mteja sahihi, kuandaa ujumbe unaoeleweka, kutumia picha na video zenye ujumbe unao eleweka kwa mteja, kupanga bajeti, kupima matokeo, kujaribu matangazo, kuwafikia tena wateja na kukuza kile kinachofanya kazi.
Kwa kifupi, NGOME YA BIASHARA ZA MTANDAONI inakusaidia kuangalia matangazo yako kwa macho tofauti.
Badala ya kusema “Nimeweka tangazo, sasa nasubiri nione.”
Utaanza kujua na kuelewa
Namtangazia nani?
Nimwambie nini?
Nitumie kiasi gani?
Nipime nini?
Nibadilishe nini?
Na nikiona tangazo linafanya kazi, nilikuze vipi?
Huo ndio ujuzi unaopata ndani ya kurasa 300 za NGOME YA BIASHARA ZA MTANDAONI.
Bei ya kawaida ya kitabu ni
SOFT COPY (PDF) Tsh 30,000/=
HARD COPY Tsh 40,000/=
Lakini kwa wateja 30 wa kwanza, utapata bei maalum ya punguzo
SOFT COPY Tsh 20,000/=
HARD COPY Tsh 35,000/=
Na wale wateja waliyo nje ya Dar es salaam wanaotaka Hard Copy wataongeza Tsh 10,000/= Kama gaharama ya usafiri wa kutumiwa kitabu hiki.
Bei hii ni maalumu kwa watu 30 wa kwanza pekee.
Baada ya nafasi hizo kuisha, bei itarudi kwenye bei ya kawaida.
Hilo si tatizo.
Kitabu kimeandikwa kwa lugha rahisi ili kukusaidia kuelewa dhana muhimu hatua kwa hatua.
Huhitaji kuwa mtaalamu wa kompyuta.
Huhitaji kuwa mtaalamu wa teknolojia (IT expert).
Unachohitaji ni simu au kompyuta, nidhamu ya kujifunza na utayari wa kutumia maarifa utakayopata baada ya kujifunza.
Usiogope Meta Ads kwa sababu hujawahi kuitumia.
Anza kujifunza.
Elewa
Fanya mazoezi.
Kisha boresha.
Sitaki kukuahidi kwamba ukinunua kitabu hiki, kesho utapata mauzo mara 5 bila kujali biashara yako.
Hilo si jambo la kweli.
Hakuna kitabu kinachoweza kudhibiti soko, bidhaa, bei, ushindani na utekelezaji wako.
Lakini kitabu hiki kinaweza kukusaidia kujenga maarifa ambayo yanakupa uwezo wa kufanya maamuzi bora zaidi kuhusu matangazo yako ya kulipia.
Lengo ni moja
Usitumie pesa kwenye matangazo bila kujua unachotafuta.
Kama una biashara mtandaoni…
Kama unatumia Facebook au Instagram kutafuta wateja…
Kama unatengeneza video za biashara yako…
Kama umejaribu matangazo lakini matokeo hayaridhishi…
Au kama bado hujaanza kwa sababu hujui pa kuanzia…
Usiendelee kubahatisha. Jenga ujuzi.
Nunua ngome ya biashara za kidigitali
Soft Copy: Tsh 20,000/=
Hard Copy: Tsh 35,000/= + Tsh 10,000/= usafirishaji kwa watu wa mkoani
Lipa kupitia mitandao ya simu, mara baada ya kulipia utapata kiunganishi au Link, na Baada ya kupata hiyo link Utapakua / Kudownload kitabu
Kwa sababu “baadaye” inaweza kuendelea kuwa kesho na kesho ikawa wiki ijayo…
wakati wewe bado unaweka pesa kwenye matangazo bila kuelewa kinachoendelea.
Watu 20 wa kwanza bado wana nafasi ya kupata bei maalum.
Nataka soft copy kwa Tsh 20,000/=
Nataka hard copy kwa Tsh 35,000/=
Huenda kwa sasa huna Tsh 20,000/=.
Au bado unataka kwanza ujifunze kidogo kabla ya kuamua.
Nimekuandalia kitu cha bure.
MFUMO WA KUNASA WATEJA
Acha kutafuta wateja kila siku. Jenga mfumo wa kuwapata, unaoongeza mauzo na unaokuza biashara yako bila kutegemea juhudi zako za kila dakika.
Ni kitabu cha bure kinachokupa mwanzo wa kuelewa namna ya kujenga mfumo wa kuwafikia na kuwabadilisha watu kuwa wateja.
Anza na hiki cha bure.
Na ukishakuwa tayari kujifunza kwa kina kuhusu matangazo ya kulipia, unaweza kurudi kwenye NGOME YA BIASHARA ZA KIDIGITALI
Kama kuna jambo ambalo hujaliona hapa, usinunue ukiwa na mashaka.
Uliza kwanza.
Lengo si kukushawishi kununua kitabu ambacho hukihitaji.
Lengo ni kukusaidia ujue kama NGOME YA BIASHARA ZA KIDIGITALI ni mwongozo unaofaa kwa hatua uliyonayo kwenye biashara yako.
NGOME YA BIASHARA ZA KIDIGITALI
Soft Copy: Tsh 20,000/= kwa watu 20 wa kwanza
Hard Copy: Tsh 35,000/= kwa watu 20 wa kwanza
+ Tsh 10,000/= usafirishaji kwa Hard Copy
Baada ya kulipia utapata kiunganishi au Link na utafungua na kudownload kitabu hicho
Usiweke pesa kwenye matangazo bila kujua unachotafuta.
Jenga ujuzi wa kuelewa unachofanya.